<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><lyrics>[V1]
 Mwokozi umeokoa,
 Nimekuwa wako wewe.
 Damu imenisafisha.
 Sifa kwa mwana Kondoo.

[V2]
 Utukufu, Aleluya!
 Sifa kwa Mwana Kondoo!
 Damu imenisafisha,
 Utukufu kwa Yesu!

[V3]
 Nilijitahidi sana
 Ila sikupata raha;
 Bali kwa kumtegemea
 Nilipata Baraka.

[V4]
 Daima namwegemea
 Damu ikifanya kazi,
 Nikioga kwa chemichemi
 Itokayo Mwokozi.

[V5]
 Sasa nimewekwa wakfu;
 Nitaishi kwako wewe:
 Fahari nashuhudia
 Ya wokovu wa bure.

[V6]
 Nasimama kwake Yesu,
 Ameponya roho yangu;
 Ameniondoa dhambi,
 Anifanye mzima.

[V7]
 Nilikuwa kifungoni,
 Niliteswa na dhambi,
 Nilifungwa minyororo
 Yesu akanifungua.

[V8]
 Sifa, ameninunua!
 Sifa, nguvu za wokovu!
 Sifa, Bwana huhifadhi!
 Sifa zake milele.</lyrics>
<title>Mwokozi Umeokoa TZR1</title>
<hymn_number>1</hymn_number>
</song>